Javascript must be enabled to continue!
Mhusika Sauti katika Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Said A. Mohamed
View through CrossRef
Makala haya yanalenga kudadisi sauti na uhusika wake kwenye uwasilishaji wa ujumbe katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Said A. Mohamed (2011). Sauti kama mojawapo ya vipengele vya utendaji imetumiwa katika kazi tofautitofauti za tamthilia kwa sababu mbalimbali kutegemea mahitaji ya mtunzi wa kazi ya sanaa. Sauti inaweza kutekeleza jukumu kubwa inaposhirikishwa vilivyo katika tamthilia. Hata hivyo, watunzi wengi wanatumia sauti kwa ajili ya kushereheshea jambo fulani, kusisitizia ujumbe na kutoa maoni kuhusu wazo kuu linalolengwa hadhira. Wakati mwingine sauti huwa inatumika kama kicheko au kuweka utangulizi na kuhitimishia tamthilia. Kwa kuzingatia matumizi hayo, ni bayana kuwa matumizi ya sauti katika tamthilia nyingi bado hayajapewa uzito unaostahili. Kutokana na hali hiyo makala haya yanachunguza namna sauti ilivyotumika kama mhusika na uwasilishaji ujumbe kwa kurejelea tamthilia ya Kimya Kimya Kimya. Hivyo, mbinu iliyotumika kukusanya data za utafiti huu ni usomaji wa kina wa tamthiliya tajwa. Hii ni tamthilia ya kipekee katika matumizi ya sauti, ambapo mwandishi Said A. Mohamed amewajenga baadhi ya wahusika wake kama wahusika sauti. Amezifanya sauti sio tu kuongea bali pia kushiriki kikamilifu katika majibizano na uigizaji na wahusika wengine. Tumezingatia jinsi sauti ilivyotumika kujenga na kukuza wahusika na uhusika katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya kwa kujikita katika ushiriki wa mhusika binafsi, uhusika wa makundi na njia zinazotumiwa na wahusika sauti kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa na mwandishi. Hatimaye, tumetathmini mchango wa sauti hizi katika kufanikisha utendaji na uwasilishaji maudhui kwa hadhira lengwa.
Title: Mhusika Sauti katika Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Said A. Mohamed
Description:
Makala haya yanalenga kudadisi sauti na uhusika wake kwenye uwasilishaji wa ujumbe katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Said A.
Mohamed (2011).
Sauti kama mojawapo ya vipengele vya utendaji imetumiwa katika kazi tofautitofauti za tamthilia kwa sababu mbalimbali kutegemea mahitaji ya mtunzi wa kazi ya sanaa.
Sauti inaweza kutekeleza jukumu kubwa inaposhirikishwa vilivyo katika tamthilia.
Hata hivyo, watunzi wengi wanatumia sauti kwa ajili ya kushereheshea jambo fulani, kusisitizia ujumbe na kutoa maoni kuhusu wazo kuu linalolengwa hadhira.
Wakati mwingine sauti huwa inatumika kama kicheko au kuweka utangulizi na kuhitimishia tamthilia.
Kwa kuzingatia matumizi hayo, ni bayana kuwa matumizi ya sauti katika tamthilia nyingi bado hayajapewa uzito unaostahili.
Kutokana na hali hiyo makala haya yanachunguza namna sauti ilivyotumika kama mhusika na uwasilishaji ujumbe kwa kurejelea tamthilia ya Kimya Kimya Kimya.
Hivyo, mbinu iliyotumika kukusanya data za utafiti huu ni usomaji wa kina wa tamthiliya tajwa.
Hii ni tamthilia ya kipekee katika matumizi ya sauti, ambapo mwandishi Said A.
Mohamed amewajenga baadhi ya wahusika wake kama wahusika sauti.
Amezifanya sauti sio tu kuongea bali pia kushiriki kikamilifu katika majibizano na uigizaji na wahusika wengine.
Tumezingatia jinsi sauti ilivyotumika kujenga na kukuza wahusika na uhusika katika tamthilia ya Kimya Kimya Kimya kwa kujikita katika ushiriki wa mhusika binafsi, uhusika wa makundi na njia zinazotumiwa na wahusika sauti kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa na mwandishi.
Hatimaye, tumetathmini mchango wa sauti hizi katika kufanikisha utendaji na uwasilishaji maudhui kwa hadhira lengwa.
Related Results
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Uchanganuzi Linganishi Wa Malezi Ya Watoto Katika Michezo Ya Kuigiza Ya Kigezi Universal Actors Na Ya Jamii Halisi
Uchanganuzi Linganishi Wa Malezi Ya Watoto Katika Michezo Ya Kuigiza Ya Kigezi Universal Actors Na Ya Jamii Halisi
Katika tasnifu hii mtafiti ameonyesha malezi ya watoto na jinsi yanavyoshughulikiwa na wahusika katika michezo ya kuigiza ya Kigezi Universal Actors ambayo ina mkusanyiko wa michez...
Pooled analysis of WHO Surgical Safety Checklist use and mortality after emergency laparotomy
Pooled analysis of WHO Surgical Safety Checklist use and mortality after emergency laparotomy
Abstract
Background
The World Health Organization (WHO) Surgical Safety Checklist has fostered safe practice for 10 years, yet i...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Global economic burden of unmet surgical need for appendicitis
Global economic burden of unmet surgical need for appendicitis
Abstract
Background
There is a substantial gap in provision of adequate surgical care in many low- and middle-income countries. ...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...

