Javascript must be enabled to continue!
Makosa Ya Kisarufi Katika Makala Andishi Za Habari: Uchunguzi Kifani Wa BBC Swahili Na DW Kiswahili
View through CrossRef
Ikisiri
Tafiti juu ya matumizi ya lugha katika vyombo vya habari zimethibitisha kuwapo kwa makosa kadhaa ya lugha katika utoaji wa habari. Makala haya, yanamakinikia makosa ya kisarufi katika matini andishi za habari za BBC Swahili na DW Kiswahili. Sampuli ya makala kumi kutoka kila tovuti ya chombo husika zilichanganuliwa kulingana na nadharia ya Corder (1967). Makosa ya udondoshaji, uchopekaji, upatanisho wa kisarufi, umoja na wingi, mpangilio wa vipashio na mantiki yalithibitika. Sababu za kufanyika kwa makosa hayo ni pamoja na: kutomudu sarufi ya Kiswahili, kukosa umakini katika uandishi na uhariri, athari za lugha mama, lugha za kigeni, lugha ya mazungumzo, na uteuzi mbaya wa msamiati. Vilevile, ilibainika kuwa makosa hayo yana athari hasi kwa wazungumzaji wa lugha pamoja na lugha yenyewe. Hata hiyo, tafiti zaidi zinapaswa kufanywa juu ya mazingira yachocheayo uvumilivu wa makosa ya lugha katika utangazaji wa habari kwa Kiswahili.
Title: Makosa Ya Kisarufi Katika Makala Andishi Za Habari: Uchunguzi Kifani Wa BBC Swahili Na DW Kiswahili
Description:
Ikisiri
Tafiti juu ya matumizi ya lugha katika vyombo vya habari zimethibitisha kuwapo kwa makosa kadhaa ya lugha katika utoaji wa habari.
Makala haya, yanamakinikia makosa ya kisarufi katika matini andishi za habari za BBC Swahili na DW Kiswahili.
Sampuli ya makala kumi kutoka kila tovuti ya chombo husika zilichanganuliwa kulingana na nadharia ya Corder (1967).
Makosa ya udondoshaji, uchopekaji, upatanisho wa kisarufi, umoja na wingi, mpangilio wa vipashio na mantiki yalithibitika.
Sababu za kufanyika kwa makosa hayo ni pamoja na: kutomudu sarufi ya Kiswahili, kukosa umakini katika uandishi na uhariri, athari za lugha mama, lugha za kigeni, lugha ya mazungumzo, na uteuzi mbaya wa msamiati.
Vilevile, ilibainika kuwa makosa hayo yana athari hasi kwa wazungumzaji wa lugha pamoja na lugha yenyewe.
Hata hiyo, tafiti zaidi zinapaswa kufanywa juu ya mazingira yachocheayo uvumilivu wa makosa ya lugha katika utangazaji wa habari kwa Kiswahili.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...