Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili

View through CrossRef
Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao. Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.A Mohamed.  Utafiti unaonyesha kwamba vijana kote duniani sasa wana utamaduni wao ambao watafiti wanaueleza kama ‘ulimwengu huru’ wa vijana ulio na mitindo na njia za maisha ambazo, vijana hufuata ili kujitofautisha na utamaduni wa wazazi wao. Utamaduni wa vijana kwa kiasi kikubwa ni zao la maendeleo katika jamii za ulimwengu. Kadri jamii inavyosonga mbele kimaendeleo, ndivyo ambavyo utamaduni wa vijana unakuzwa, unaimarishwa na kusambazwa miongoni mwa vijana kote duniani. Vijana wamebuni utamaduni wao kama njia moja ya kuasi dhidi ya utamaduni uliotawaliwa na wazee. Wanataka kujihusisha na tabia kama matumizi ya dawa za kulevya, ushoga, uasi wa maadili ya kijamii, Mitindo mipya ya mavazi, muziki miongoni mwa tabia nyingine ambazo wanajua huwatenga wazee. Hii ni tabia ibuka ya vijana kupania kuonyesha nguvu na uwezo wao katika jamii. Ujumbe wanaopitisha ni kuwa hawako tayari kushiriki utamaduni unaowadhibiti na kuwanyima nafasi yao katika jamii. Malengo mahususi yatakayoongoza makala haya ni pamoja na kuangazia sifa za vijana wa kisasa na wakati huo huo kufafanua njia mabazo wanajamii wanaweza kutumia ili kujaribu kuziba mwanya mpana uliopo kati ya kizazi cha jana na cha leo. Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia. Mhimili mkuu wa nadharia ya uhalisia ambao utaongoza makala ni kwamba, fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kumulika maisha kama yalivyo. Muundo wa kimaelezo utatumika kuchanganua data. Data itakusanywa kutokana na kusoma riwaya teule na kudondoa sehemu zinazolingana na malengo ya utafiti. Data itadondolewa, itanukuliwa, itapangwa kisha kuchanganuliwa kulingana na mada husika
Title: Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili
Description:
Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao.
Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.
A Mohamed.
  Utafiti unaonyesha kwamba vijana kote duniani sasa wana utamaduni wao ambao watafiti wanaueleza kama ‘ulimwengu huru’ wa vijana ulio na mitindo na njia za maisha ambazo, vijana hufuata ili kujitofautisha na utamaduni wa wazazi wao.
Utamaduni wa vijana kwa kiasi kikubwa ni zao la maendeleo katika jamii za ulimwengu.
Kadri jamii inavyosonga mbele kimaendeleo, ndivyo ambavyo utamaduni wa vijana unakuzwa, unaimarishwa na kusambazwa miongoni mwa vijana kote duniani.
Vijana wamebuni utamaduni wao kama njia moja ya kuasi dhidi ya utamaduni uliotawaliwa na wazee.
Wanataka kujihusisha na tabia kama matumizi ya dawa za kulevya, ushoga, uasi wa maadili ya kijamii, Mitindo mipya ya mavazi, muziki miongoni mwa tabia nyingine ambazo wanajua huwatenga wazee.
Hii ni tabia ibuka ya vijana kupania kuonyesha nguvu na uwezo wao katika jamii.
Ujumbe wanaopitisha ni kuwa hawako tayari kushiriki utamaduni unaowadhibiti na kuwanyima nafasi yao katika jamii.
Malengo mahususi yatakayoongoza makala haya ni pamoja na kuangazia sifa za vijana wa kisasa na wakati huo huo kufafanua njia mabazo wanajamii wanaweza kutumia ili kujaribu kuziba mwanya mpana uliopo kati ya kizazi cha jana na cha leo.
Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia.
Mhimili mkuu wa nadharia ya uhalisia ambao utaongoza makala ni kwamba, fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kumulika maisha kama yalivyo.
Muundo wa kimaelezo utatumika kuchanganua data.
Data itakusanywa kutokana na kusoma riwaya teule na kudondoa sehemu zinazolingana na malengo ya utafiti.
Data itadondolewa, itanukuliwa, itapangwa kisha kuchanganuliwa kulingana na mada husika.

Related Results

Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili
Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili
Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao. Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.A Mohamed.  Utafit...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...

Back to Top