Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Uchunguzi wa Ikolojia-Ubeberu katika Fasihi ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Nakuruto ya Clara Momanyi

View through CrossRef
Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, fasihi ya Kiswahili imekuwa ikitoa mchango mkubwa kuhusu masuala ya mazingira kupitia tanzu mbalimbali za fasihi andishi na fasihi simulizi. Miongoni mwa kazi za kwanzakwanza kushughulikia suala la mazingira katika fasihi ya Kiswahili nchini Kenya ni riwaya ya Nakuruto (2009) ya Clara Momanyi. Riwaya ya Nakuruto ilitungwa wakati ambapo kazi za fasihi ya kimazingira zilikuwa haba. Makala hii inalenga kuchunguza jinsi riwaya hii inavyokosoa ubeberu dhidi ya mazingira uliofanywa na wakoloni na wenyeji. Shughuli za unyonyaji wa rasilimali za wenyeji kwa manufaa ya Wamagharibi na wenyeji zimechunguzwa pia. Riwaya ya Nakuruto iliteuliwa kimakusudi ili kuchunguza suala la ikolojia-ubeberu. Mbinu ya ukusanyaji data ya usomaji makini wa riwaya teule ilitumiwa, data ilinakiliwa na kutiwa katika mada ndogondogo. Mtafiti alinukuu madondoo yanayolenga suala la ikolojia-ubeberu katika riwaya, akayafasiri na kunukuu wanayoyasema wasomi wengine kuhusu suala hilo huku akiongozwa na Nadharia ya Uhakiki-ikolojia. Matokeo ya utafiti yalionesha bayana kwamba binadamu huyatawala na kuyaharibu mazingira kiasi cha kuhatarisha uhai katika sayari. Mwanadamu amekuwa akinyonya maliasili na kuonesha sifa za ubeberu zilizojaa choyo, ubinafsi na tamaa katika harakati yake ya kujinufaisha kutokana na maliasili ambayo inajumlisha vyanzo vya maji, milima, udongo, madini pamoja na miti.
University of Dar es Salaam
Title: Uchunguzi wa Ikolojia-Ubeberu katika Fasihi ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Nakuruto ya Clara Momanyi
Description:
Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, fasihi ya Kiswahili imekuwa ikitoa mchango mkubwa kuhusu masuala ya mazingira kupitia tanzu mbalimbali za fasihi andishi na fasihi simulizi.
Miongoni mwa kazi za kwanzakwanza kushughulikia suala la mazingira katika fasihi ya Kiswahili nchini Kenya ni riwaya ya Nakuruto (2009) ya Clara Momanyi.
Riwaya ya Nakuruto ilitungwa wakati ambapo kazi za fasihi ya kimazingira zilikuwa haba.
Makala hii inalenga kuchunguza jinsi riwaya hii inavyokosoa ubeberu dhidi ya mazingira uliofanywa na wakoloni na wenyeji.
Shughuli za unyonyaji wa rasilimali za wenyeji kwa manufaa ya Wamagharibi na wenyeji zimechunguzwa pia.
Riwaya ya Nakuruto iliteuliwa kimakusudi ili kuchunguza suala la ikolojia-ubeberu.
Mbinu ya ukusanyaji data ya usomaji makini wa riwaya teule ilitumiwa, data ilinakiliwa na kutiwa katika mada ndogondogo.
Mtafiti alinukuu madondoo yanayolenga suala la ikolojia-ubeberu katika riwaya, akayafasiri na kunukuu wanayoyasema wasomi wengine kuhusu suala hilo huku akiongozwa na Nadharia ya Uhakiki-ikolojia.
Matokeo ya utafiti yalionesha bayana kwamba binadamu huyatawala na kuyaharibu mazingira kiasi cha kuhatarisha uhai katika sayari.
Mwanadamu amekuwa akinyonya maliasili na kuonesha sifa za ubeberu zilizojaa choyo, ubinafsi na tamaa katika harakati yake ya kujinufaisha kutokana na maliasili ambayo inajumlisha vyanzo vya maji, milima, udongo, madini pamoja na miti.

Related Results

Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Kila mtoto huhitaji malezi thabiti katika maisha ili kumkuza katika uadilifu wa siku za baadaye. Utafiti huu ulishughulikia maudhui ya malezi ya watoto kwa kuegemea fasihi ya watot...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

Back to Top