Javascript must be enabled to continue!
Athari ya Upokezi wa Matendo ya Utu kwa Binadamu: Mfano wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed
View through CrossRef
Ili pawepo na mahusiano mema kati ya binadamu, lazima pawepo na utu. Utu, hasa huhusishwa na binadamu. Hali kadhalika, huhusisha wema wowote unaomtendea mtu. Waandishi mbalimbali wa fasihi ya Kiswahili wamedhihirisha utu katika utunzi wao. Mtu anapopokea tendo la utu, huathirika kwa namna mbalimbali. Makala haya yanachunguza athari ya upokezi wa matendo ya utu kwa binadamu. Lengo kuu la makala ni kueleza binadamu anavyoathirika kwa njia mbalimbali kutokana na utu wa viumbe wa kiuhalisiajabu. Viumbe wa kiuhalisiajabu kama wanavyoitwa ni viumbe wenye sifa za kiajabuajabu. Ni viumbe tofauti na binadamu halisi na wenye nguvu fulani. Kutokana na nguvu hizo, huweza kufanya matendo mbalimbali. Makala iliongozwa na nadharia ya kiuhalisiajabu kama inavyofafanuliwa na Zamora na Wendy (1995). Muundo wa kimaelezo ulitumika huku eneo la utafiti likiwa fasihi ya Kiswahili, utanzu wa Riwaya. Sampuli ya kimakusudi ilitumika kuteua riwaya tatu za Said A. Mohamed hususan: Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Data ilikusanywa kutokana na kusoma riwaya hizo tatu zilizoteuliwa na kudondoa sehemu zilizolingana na malengo ya utafiti. Data ilidondolewa, ikanukuliwa, ikapangwa kisha kuchanganuliwa. Matokeo yalionyesha kuwa viumbe wa kiuhalisiajabu walidhihirisha utu kwa binadamu kwa namna mbalimbali na athari yake ikabainika. Utafiti huu unatoa mchango kwa walimu na wataalamu wa fasihi katika taaluma ya fasihi simulizi.
Title: Athari ya Upokezi wa Matendo ya Utu kwa Binadamu: Mfano wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed
Description:
Ili pawepo na mahusiano mema kati ya binadamu, lazima pawepo na utu.
Utu, hasa huhusishwa na binadamu.
Hali kadhalika, huhusisha wema wowote unaomtendea mtu.
Waandishi mbalimbali wa fasihi ya Kiswahili wamedhihirisha utu katika utunzi wao.
Mtu anapopokea tendo la utu, huathirika kwa namna mbalimbali.
Makala haya yanachunguza athari ya upokezi wa matendo ya utu kwa binadamu.
Lengo kuu la makala ni kueleza binadamu anavyoathirika kwa njia mbalimbali kutokana na utu wa viumbe wa kiuhalisiajabu.
Viumbe wa kiuhalisiajabu kama wanavyoitwa ni viumbe wenye sifa za kiajabuajabu.
Ni viumbe tofauti na binadamu halisi na wenye nguvu fulani.
Kutokana na nguvu hizo, huweza kufanya matendo mbalimbali.
Makala iliongozwa na nadharia ya kiuhalisiajabu kama inavyofafanuliwa na Zamora na Wendy (1995).
Muundo wa kimaelezo ulitumika huku eneo la utafiti likiwa fasihi ya Kiswahili, utanzu wa Riwaya.
Sampuli ya kimakusudi ilitumika kuteua riwaya tatu za Said A.
Mohamed hususan: Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010).
Data ilikusanywa kutokana na kusoma riwaya hizo tatu zilizoteuliwa na kudondoa sehemu zilizolingana na malengo ya utafiti.
Data ilidondolewa, ikanukuliwa, ikapangwa kisha kuchanganuliwa.
Matokeo yalionyesha kuwa viumbe wa kiuhalisiajabu walidhihirisha utu kwa binadamu kwa namna mbalimbali na athari yake ikabainika.
Utafiti huu unatoa mchango kwa walimu na wataalamu wa fasihi katika taaluma ya fasihi simulizi.
Related Results
Impact of opioid-free analgesia on pain severity and patient satisfaction after discharge from surgery: multispecialty, prospective cohort study in 25 countries
Impact of opioid-free analgesia on pain severity and patient satisfaction after discharge from surgery: multispecialty, prospective cohort study in 25 countries
Abstract
Background
Balancing opioid stewardship and the need for adequate analgesia following discharge after surgery is challe...
Predicting opioid consumption after surgical discharge: a multinational derivation and validation study using a foundation model
Predicting opioid consumption after surgical discharge: a multinational derivation and validation study using a foundation model
Abstract
Opioids are frequently overprescribed after surgery. We applied a tabular foundation model to predict the risk of post-discharge opioid consumption. The model wa...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe...
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Kila mtoto huhitaji malezi thabiti katika maisha ili kumkuza katika uadilifu wa siku za baadaye. Utafiti huu ulishughulikia maudhui ya malezi ya watoto kwa kuegemea fasihi ya watot...
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Utafiti huu unalenga kuchunguza kwa kina nafasi na athari za mwandishi anaposhiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutafsiri kazi yake ya kifasihi, kwa kuzingatia tamthilia mbili...
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi san...
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ng...