Javascript must be enabled to continue!
Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi
View through CrossRef
Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha utawala wa viongozi mintarafu ya riwaya teule. Ili kutimiza lengo lake, mtafiti amehakiki riwaya nne: Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Nadharia ya hejemonia inayoweka wazi suala la utawala wa mabwanyenye juu ya raia na kueleza udumishaji wa uwezo na mamlaka juu ya watawaliwa ni mwafaka katika utafiti huu. Mintarafu ya nadharia hii, hejemonia huendelezwa na kudumishwa sio tu kwa ushurutishaji bali pia kupitia maafikiano, lugha, wataalamu, siasa, maagizo, burudani, ujumbe na nyenzo nyingine za kielimu. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi kwa kudhamiria kuwa zimesheheni masuala ya uhimili wa hejemonia. Kutokana na riwaya hizo, mtafiti alipata mitazamo mipana na tofauti ya propaganda kwa mujibu wa nguzo za nadharia na madhumuni ya utafiti. Utafiti huu ni wa maktabani ambako usomi mpana na wa kina wa riwaya teule, vitabu vya ziada, majarida na tasnifu mbalimbali ulitekelezwa. Utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kiuthamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Muundo wa kimaelezi ulitumika kuchanganua data na kueleza matukio kwa uyakinifu. Utafiti umeonesha kuwa propaganda ni mkakati muhimu unaotumiwa na watu wenye uwezo na mamlaka kudumisha na kuhimili hejemonia katika jamii. Matokeo ya utafiti yanatoa maarifa zaidi kuhusu matumizi ya propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika fasihi. Aidha, matokeo haya ni marejeleo muhimu kwa wahakiki na watafiti hususan wale wanaotafitia masuala ya hejemonia katika fasihi
East African Nature and Science Organization
Title: Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi
Description:
Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili.
Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha utawala wa viongozi mintarafu ya riwaya teule.
Ili kutimiza lengo lake, mtafiti amehakiki riwaya nne: Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi.
Nadharia ya hejemonia inayoweka wazi suala la utawala wa mabwanyenye juu ya raia na kueleza udumishaji wa uwezo na mamlaka juu ya watawaliwa ni mwafaka katika utafiti huu.
Mintarafu ya nadharia hii, hejemonia huendelezwa na kudumishwa sio tu kwa ushurutishaji bali pia kupitia maafikiano, lugha, wataalamu, siasa, maagizo, burudani, ujumbe na nyenzo nyingine za kielimu.
Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi kwa kudhamiria kuwa zimesheheni masuala ya uhimili wa hejemonia.
Kutokana na riwaya hizo, mtafiti alipata mitazamo mipana na tofauti ya propaganda kwa mujibu wa nguzo za nadharia na madhumuni ya utafiti.
Utafiti huu ni wa maktabani ambako usomi mpana na wa kina wa riwaya teule, vitabu vya ziada, majarida na tasnifu mbalimbali ulitekelezwa.
Utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kiuthamano ikitumika kuchanganua data hiyo.
Muundo wa kimaelezi ulitumika kuchanganua data na kueleza matukio kwa uyakinifu.
Utafiti umeonesha kuwa propaganda ni mkakati muhimu unaotumiwa na watu wenye uwezo na mamlaka kudumisha na kuhimili hejemonia katika jamii.
Matokeo ya utafiti yanatoa maarifa zaidi kuhusu matumizi ya propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika fasihi.
Aidha, matokeo haya ni marejeleo muhimu kwa wahakiki na watafiti hususan wale wanaotafitia masuala ya hejemonia katika fasihi.
Related Results
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Upole ni hali ya msemaji kudhihirisha kuwa anajali hisia na mahitaji ya msikilizaji katika mazungumzo. Mikakati ya upole hutumiwa na washiriki wa mazungumzo kulainisha na kufanikis...
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba
Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ng...
Propaganda and Lone-Actor Terrorism
Propaganda and Lone-Actor Terrorism
There exists a critical symbiotic relationship between propaganda and lone-actor terrorism. Propaganda relies on the martyrdom of lone-actor terrorists as a symbolic factor in prom...
The Role of Propaganda in Modern Society
The Role of Propaganda in Modern Society
Purpose: This study aimed to examine the historical development, theoretical foundation, and modern application of the propaganda system as a key mechanism for shaping public opini...
Rose Macaulay and Propaganda
Rose Macaulay and Propaganda
The novelist Rose Macaulay (1881–1958) had direct professional experience of Britain's secret propaganda operation during the First World War. She was among the first British novel...
Digital Propaganda and Diplomacy
Digital Propaganda and Diplomacy
Abstract
This chapter delves into the connection between digital propaganda and diplomacy, examining the political implications and epistemic position of propaganda ...
Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"
Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"
Kazi ya fasihi ikiwemo riwaya huundwa na fani na maudhui, ambavyo kwa pamoja ndivyo hutupatia kazi inayoitwa fasihi. Fani huundwa na vipengele kama vile wahusika, mtindo, mandhari,...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...

